maproo

NGOMA AWASHUKURU MASHABIKI WA YANGA

Mshambuliaji wa kimataifa wa Yanga Donald Dombo Ngoma amewashukuru mashabiki wa Yanga kwa kumchangia kiasi cha pesa kama ishara ya pole.

Mashabiki wa Yanga waliofurika uwanjani jana walitembeza ‘bakuli’ kwa ajili ya kumpa pole Ngoma aliyefiwa na mdogo wake wiki iliyopita hali iliyopelekea yeye kuukosa mchezo wa kufuzu kwa klabu bingwa Afrika dhidi Ya Cercle De Joachim.


Ngoma aliandika kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa facebook”ningependa kuwashukuru mashabiki wa Yanga kwa waliyonifanyia maneno pekee hayatoshi kuwashukuru Mungu awabariki nyote daima mbele nyuma mwiko” aliandika Ngoma

About dada

0 comments:

Powered by Blogger.