ZGPL

SHOMARI APIGILIA MISUMALI MIWILI POLISI

Mchezaji wa Timu ya Kimbunga Shomari Waziri amezidi kuwa gumzo katika ligi kuu ya Zanzibzar kanda ya Unguja baada ya jana kupachika mabao 2 walipowafunga Polisi 2-1, katika mchezo wa ligi kuu ya Zanzibar kanda ya Unguja.

Katika mchezo huo Polisi walikuwa ndio wa mwanzo kuliona lango la Kimbunga baada ya Abdallah Omar kufunga katika dakika ya 11, lakini dakika chache Shomar Waziri ndipo aliposawazisha mnamo dakika ya 20, na bao jengine akafunga katika dakika ya 54 ya mchezo huo.

Matokeo hayo yamezidi kuwaweka katika wakati ngumu timu ya Polisi kwani wamepata ushindi mechi moja katika mechi 15 walizocheza katika ligi hiyo, na kuzidi kujiweka mkiani mwa ligi hiyo wakiwa na alama nane 8.

Shomari sasa amefikisha mabao 12 katika mechi 16 walizocheza na amekuwa kinara wa kufunga magoli mengi katika ligi kuu ya Zanzibar kanda ya Unguja huku akimuwacha mpinzani wake Mbarouk Chande wa Timu ya jeshi la kujenga Uchumi Zanzibar (JKU) ambae ana magoli 9 katika ligi hiyo.

Kimbunga sasa wapo nafasi ya saba (7) na wamefikisha alama 23 wakiwa wapo alama sawa na bingwa mtetezi Klabu ya Mafunzo.

Shomari Waziri ameelezea siri yake ya ushindi na kusema kujituma ndio sababu ya kufunga mabao mengi.

“Siri ya ushindi ni kujituma na hakuna chengine, pia huu ni uwezo binafsi M/mungu amenipangia pia na kipaji cha kutia kamba ndo kawaida yangu”. Alisema Shomari.

Shomari amechezea timu za madaraja kama Korogo united ya Tanga, Ukwamani ya  Dar es Salaam na nyenginezo ,Aidha amewataka mashabiki wa kimbuga watarajie kufika nne bora na pia watarajie nafasi ya kwanza.

Kwa upande wake kocha wa timu ya Polisi Ali Suleiman Mtuli amesema kuwa mchezo ulikuwa ni mzuri lakini umekuwa ni mbaya kwa vile wamepoteza mechi hiyo.

“Mchezo haukuwa mbaya kiupande wetu lakini tumepoteza ndo maana mechi ikawa mbaya, kwa kweli timu yangu imecheza vizur lakjini wachezaji wangu bado hawajawa makini wakifika mbele na hicho ndicho kilio change na sijui kitafika wapi kwa kifupi wananiangusha katika maeneo ya ufungaji” Alisema Mtuli.

Chasnzo: salmasportmedia.blogspot.com

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.