wanawake

TWIGA STARS WALALA AZAM COMPLEX


Timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania, Twiga stars leo wamepoteza mbele ya Zimbabwe kwa goli 2-1 katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa Azam complex.

Katika mchezo huo wa kusaka tiketi ya kushiriki kombe la mataifa Afrika, Zimbabwe walianza mchezo kwa kasi na kutawala vilivyo kwa dakika kumi za mwanzo kabla ya Twiga kuanza kuutawala mchezo.

Twiga stars ndio walikuwa wa mwanzo kupata goli kupitia kwa Mwanahamisi Omari katika dakika ya 17 kabla ya Zimbabwe kusawazisha katika dakika ya 19 kupitia kwa Erina Jeke.

Kuingia kwa magoli hayo kulipelekea timu kucheza kwa kujihami na kila upande wakitegemea mashambulizi ya kushtukiza, na mpaka dakika 45 za mwanzo zinakamilika matokeo yalikuwa 1-1.

Kipindi cha pili Zimbabwe walirejea kwa kasi na katika dakika ya 47 Erina Jeke aliiandikia Zimvabwe goli la pili na kupelekea mchezo kumalizika kwa Zimbabwe kuibuka na ushindi wa goli 2-1.

Twiga stars watarejeana na Zimbabwe wiki mbili zijazo nchini Zimbabwe, huku wakitakiwa kupata ushindi wa tofauti ya goli 2 iliwatinge hatua inayofuata.

About dada

0 comments:

Powered by Blogger.