zanzibar

UCHAGUZI WA ZFA TAIFA KUFANYIKA APRIL 14

Kamati ya Uchaguzi ya chama cha soka Zanzibar (ZFA) imetangaza rasmi tarehe ya kufanyika uchaguzi wa ZFA ambao unatarajiwa kufanyika tarehe 14 mwezi ujao wa April.

Akizungumza na Mtandao huu katibu wa kamati hiyo Afaan Othman alisema uchaguzi utafanyika kisiwani Pemba tarehe 14 April saa 4:00 asubuhi.

“ Tunategemea kufanya uchaguzi tarehe 14/04/2016 Kisiwani Pemba, tunaweza kuufanya Gombani au kule Wesha Pwani”.

Aidha Affan amewataka wadau mbali mbali wa soka wajitokeze kuchukua fomu za kugambania nafasi tatu zitakazogombaniwa katika uchaguzi huo ambazo ni Urais wa ZFA, Makamu wa Urais ZFA Unguja na Makamu wa Urais ZFA Pemba ambapo fomu za kugombania zitauzwa shs laki mbili.

“ Kwa wale wenye nia ya kuchukua fomu nawaomba wajitokeze kwa wingi ili waje kuongoza soka la Zanzibar”.

Wakati huo huo kamati hiyo imezitaja Sifa 6 za kugombea nafasi hizo tatu kwenye uchaguzi huo.

1. Mgombea awe Mzanzibari.
2. Mgombea awe na elimu kiwango cha kidato cha nne.
3. Mgombea awe na umri usiopungua miaka 30.
4. Mgombea awe na uzoefu wa kuongoza soka.
5. Mgombea asiwe mtu aliefungwa jela kwa kosa jinai.
6. Mgombea awe na akili timamu.

Pia kamati hiyo imetangaza siku za kuchukua fomu ambazo zitaanza rasmi kuuzwa kesho tarehe 27/03/2016 na mwisho wa kuchukua fomu ni tarehe 06/04/2016 ambapo pia tarehe 07/04/2016 itakuwa ni siku ya usaili.

Fomu za uchaguzi kwa upande wa kisiwa cha Unguja zitauzwa na Suleiman Haji (Kibabu) ambae ni mwenyekiti wa kamati hiyo, na kule kisiwani Pemba fomu zitauzwa na Affan Othman ambae ni Katibu wa kamati hiyo.

Kamati hiyo ina jumla ya wajumbe wa nne (4) ambao ni Khamis Suleiman pamoja na Mmanga Mjaka wakiongozwa na Suleiman Haji (Kibabu) ambae ni mwenyekiti na Affan Othman ambae ni Katibu wa kamati hiyo.

Katiba ya ZFA ya mwaka 2010 ndio itakayotumika katika zoezi zima hilo la uchaguzi ambapo mtu yoyote atakaechukua fomu hatoredeshewa fedha zake hata kama atajitoa kushiriki uchaguzi huo.

Chanzo: Salma Sports

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.