Katika mchezo huo ulioshuhudia yanga wakingoja mpaka dakika ya 26 kupata goli la kuongoza baada ya Ndanda FC kuwadhibiti vyema viongo vya yanga katika dakika hizo 25, na goli la yanga lilifungwa na Paul Nonga kwa kichwa akiunga mpira wa adhabu.
Kuingia kwa goli hilo kuliwapa utawala yanga SC na kujaribu kutengeneza nafasi kadhaa za goli ambazo hazikuzaa matunda na kupeleka mchezo kwenda mapumziko yanga wakiwa mbele kwa goli 1-0.
Kipindi cha pili kilirejea kwa kasi huku Ndanda FC wakisaka goli la kusawzisha na wakiimarisha eneo lao la ulinzi kitendo kilichopeleka yanga sc kushindwa kuongeza goli al pili.
Katika dakika ya 56 kiungo aliyepata kupitia yanga sc, Kigi Makasi aliiandikia Ndanda FC goli la kusawazisha na kupeleka yanga sc kuongeza kasi yao ya ushambuliaji huku Ndanda FC wakituma mipira ya kushtukiza.
Katika dakika ya 68 Paul Ngalema alizawadiwa kadi nyekundu kwa kosa la kumuangusha Saimon Msuva katika eneo la hatari, na beki Kelvin Yondani akaindika Yanga SC goli la pili kwa mkwaju wa penati.
Kuingia kwa goli hilo kuliongeza umakini kwa Yanga SC na kuwamaliza Ndanda FC na kupeleka mchezo kumalzika kwa Yanga SC kuibuka na ushindi wa goli 2-1.
Yanga SC inaungana na Azam FC, na Mwadui FC katika hatua ya nusu fainali inayotazamiwa kuchezwa mwishoni mwa mwezi huu, huku mchezo wa mwisho katika hatua ya robo fainali ikitarajiwa kuchezwa aprili 11 katika ya Simba SC na Coastal union katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.a
0 comments:
Post a Comment