Mchezo huo uliosukumwa ndani ya dimba la Amani majira ya saa kumi za jioni, timu hizo zilicheza kwa kila timu kutaka kuondoka na ushindi lakini hadi dakika 90 zinamalizika hakuna timu iliyoona lango la mwenzake.
Katika mtanange huo mnamo dakika ya 66 mwamuzi Rashid Farghan aliwatoa nje kwa kuwaonesha kadi nyekundu mchezaji wa Black sailors Bakar Kuluzo pamoja na mchezaji wa Zimamoto Hassan Said, baada ya kufanyiana rafu katika mchezo huo.
SALMA SPORT’S MEDIA ilizungumza na kocha wa timu ya Black sailors Juma Awadh na akisema kuwa kukosa umakini ni tatizo la kukosa ushindi katika mchezo wa leo.
“Tumekosa umakini hususan kwa upande wa strickers kwa hiyo mambo ya mpira yanatokezea, tutafanya training kw asana nafikiri tukisawazisha haya tu kila kitu kitakaa vizuri”. Alisema kocha Awadh.
Aidha kocha msaidizi wa timu ya Zimamoto, Juma Abdul-rahiim kiupande wake amesema kuwa mchezo ulikuwa mzuri kwa timu zote.
“Mchezo ulikuwa mzuri kwa timu zote mbili, unajua timu mara ya mwanzo ukiifunga goli nne mara ya pili itakuja kujiandaa vizuri tu, nilitegemea tu kwamba Black sailors akija mara ya pili itakuwa shughuli nzito”. Alisema kocha Juma.
Matokeo haya yameifanya timu ya Zimamoto kubaki nafasi ya tatu 3 wakiwa na alama 29, na Black sailors wao wamesalia nafasi ya saba 7 na alama 26.
Chanzo: Salma Sport's Media
0 comments:
Post a Comment