ASFC

COASTAL WAIADHIBU SIMBA SC TAIFA NA KUTINGA NUSU FAINALI KOMBE LA TFF


Baada ya kutibua rikodi za kutopoteza mchezo kwa Yanga SC na Azam FC, Coastal union leo wamezima ndoto ya Simba SC kuiwakilisha Tanzania Bara katika michuano ya Kombe la shirikisho Afrika Mwakani, baada ya kuwafunga goli 2-1.

Matumaini ya Simba SC kushiriki michuano ya kimataifa mwakani yamebakia katika mbio za ubingwa wa ligi kuu, ambapo anafukuzana kwa karibu na Azam FC na Yanga.

Katika mchezo wa leo wa kombe la TFF uliochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Coastal union walikuwa wa mwanzo kupata goli kupiti kwa Yousuf Sabo kwa mpira wa adhabu aliopiga moja kwa moja na kuiandika Coastal goli la uongozi katika dakika ya 20.

Kuingia kwa goli hilo Simba SC walijaribu kufika langoni mwa Coastal union bila mafanikio yoyote katika kipindi cha kwanza na kuplekea dakika 45 za kwanza kumalizika kwa Coastal union kuibuka na ushindi wa goli 1-0.

Kipindi cha Simba SC walianza kwa mabadiliko ambapo aliingi Hamisi Kiiza na Awadh Juma kuchukuwa nafasi ya Said NDemla na Hassan Kessi.

Mabadiliko hayo yaliongeza kasi kwa Simba SC na katika dakika ya 49 Hamiisi Kiiza aliitendea vyema krosi ya Ibrahim Ajibu na kuiandikia Simba SC goli la kusawazisha.

Kuingia kwa goli ilo kulipeleka kocha Ally Jangalu kumuinua kwenye benchi Ahmad Ally Shiboli na kuingia uwanjani.

Simba SC waliendelea kushambulia kwa kasi uku Coastal union wakitumia mipira ya kushtukiza kupitia kwa Shiboli na Mahadhi.

Katika dakika ya 84 Shiboli akiwa anaenda kumsalimu kipa wa Simba SC beki wa Simba SC Novaty Lufungo alimfanyia madhambi na mwamuzi wa mchezo huo kuamuru penati ipigwe kuelekea langoni mwa Simba SC, huku Lufungo akizawadiwa kadi nyekundu.

Sabo aliifunga penati hiyo kwa ustadi mkubwa na kuiandika Coastal union goli la pili na kupelekea Simba SC kukubali kichapo cha goli 2-1 toka kwa Coastal union.

Kwa matokeo hayo Coastal union ameungana na Azam FC, Yanga SC na Mwadui FC katika hatua ya nusu fainali ya kombe la TFF, ambapo droo yake itafanyika kesho usiku na kurushwa livie kupitia azam two.

Bingwa wa michuano hii ndio atakaei wakilisha Tanzania bara katika michuano ya kombe la shirikisho la soka Africa (CAF confederation cup) mwakani.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.