Timu ya Jeshi la Kujenga Uchumi Zanzibar JKU, imeendeleza dimbwi lake la ushindi baada ya kuwanyuka Kimbunga mabao 3-0, katika mchezo wa ligi kuu ya Zanzibar kanda ya Unguja uliosukumwa jana ndani ya uwanja wa Amani mjini Unguja.
Katika mchezo huo uliochezwa majira yan saa kumi za jioni, JKU walianza kucheza kwa kasi na kwenda kulishambulia lango la Kimbunga ndipo Emmanuel Martin alipofunga bao la kwanza katika dakika ya pili (2).
JKU iliendeleza mashambulizi na kuutawala mchezo huo takriban dakika zote za kipindi cha kwanza, pia walikosa nafasi nyingi za kushinda lakini katika dakika ya 44 Mbarouk Chande alifunga bao la pili, na kuweza kujiandikia bao la kumi (10) katika ligi hiyo huku akimfukuzia mchezaji wa Kimbunga Shomari Waziri mwenye mabao 12, ambae mchezo wa jana hakuonesha makali yake kama ilivyozoeleka.
Mnamo dakika za nyongeza za kipindi cha kwanza Emmanuel Martin alirudi tena wavuni kwa kuiandikia JKU bao la tatu (3).
Katika kipindi cha pili Kimbunga waliimarisha safu yao ya ulizi kwani hawakuruhusu bao jengine katika lango lao, na mtanange huo ulimalizika kwa JKU kuibuka na ushindi wa mabao 3-0.
Kocha wa timu ya JKU Omar Khamis kuwa wamtengeza nafasi nyingi katika mchezo huo lakini wamezitumia kidogo.
“Tumetengeza nafasi nyingi lakini tumezitumia kidogo lakini nyingi zaidi tumezikosa, kwa kweli haya yote ni kutokuwa makini, kwa sababu nafasi kama zile tungezipata tungeweza kufunga magoli kirahisi kabisa”. Alisema Omar.
Kwa upande wa Kaimu kocha wa timu ya Kimbunga Ali Khamis Tall, amesesma kuwa “kutokana na kufungwa magoli matatu kwa kweli hali ya timu yangu mumeiona hata reserve hakuna wachezaji wengi ni wagonjwa, sasa wachezaji wenyewe nimelazimisha tu kucheza”.
Kwa matokeo hayo JKU bado ni vinara wa ligi hiyo, wakiwa na alama 44, na Kimbunga wao wana alama 23 wakishika nafasi ya tisa (9).
0 comments:
Post a Comment