Matina Nkurlu-Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania |
Ufuatiliaji huu wa Vodacom umeanza siku moja baada ya kuwepo taarifa kuwa Kampuni ya Geita Gold Minning imevunja mkataba wa kuidhamini timu ya Geita Sports wenye thamani ya Tsh. milioni 300 kutokana na kukutwa na hatia kuhusishwa na upangaji matokeo katika mchezo wake wa mwisho dhidi ya JKT Kanembwa ambapo Geita ilishinda bao 8-0.
Akiongea na mtandao huu kuhusiana na sakata hilo Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu amesema kuwa, wameamua kulifuatilia kwa makini suala hili kwa kuwa ligi hiyo ndiyo inatoa timu tatu bora zinazopanda daraja na kushiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara ambao wanaidhamini.
“Tunadhamini Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara kwa lengo la kukuza mchezo wa soka nchini, tunapenda kuona malengo yetu ya kukuza soka hapa nchini yakirandana na kufuatwa kwa sheria zote za ili tuendeleze mchezo huu nchini na ngazi ya kimataifa na kuboresha maisha ya wachezaji pia mchezo kuchangia pato la serikali kupitia kodi.”
“Napenda kuwasihi viongozi wa soka kuzingatia sheria kwa umakini ili malengo haya yaliyokusudiwa yaweze kufikiwa”, alisema Nkurlu.
Chanzo: shaffihduada.co.tz
0 comments:
Post a Comment