ZGPL

MAFUNZO WAFUFUA MATUMAINI YA KUTETEA TAJI LAO


Bingwa mtetezi,timu ya Mafunzo imejipa matumaini ya kuingia hatua ya nne bora kwa upande wa Unguja, na kulitetea taji lao la ligi kuu ya Zanzibar.

Timu hiyo imeweza kufufua matumaini yao baada ya kuwafunga Maustadh wa Chuoni bao 1-0 katika mchezo wa ligi kuu ya Zanzibar kanda ya Unguja uliosukumwa ndani ya dimba la Amani hapa mjini Unguja.

Mafunzo imejipatia bao hilo lililofungwa na Moh’d Abdul-Rahiim Mbambi katika dakika ya 60 muda mchache tu alipotokea bench kwa kuchukua nafasi ya Ali Juma.

Kocha wa timu ya Mafunzo Moh’d Kachumbari amesema kuwa mchezo ulikuwa ni mzuri na kila mtu kaonesha uwezo wake.

“Mchezo ulikuwa mzuri tu kila mtu kaonesha uwezo wake lakini sie tulikuwa tunatumia sana upande wa ushambuliaji kwa sababu timu yetu sasa hivi tupo katika mambo ya umaliaziaji, tumepata goli moja lakini tumeondoka na ushindi”.Amesesma Kachumbari.

Kachumbar  aliongezeza kwa kusema, “tunafanya mazoezi kuingia katika timu za nne bora tumekusudia safari hii kuuchukua tena ubingwa kwa njia ya aina yoyote ile”.

Kwa upande wa kocha wa Chuoni Abdallah Ali, amesesma

“Mchezo tumepoteza kwanza marifa wanazibeba sana za askari,kwa sababu tumefunga goli clear refaree anasema hamna goli. Kupoteza mechi ni kama mechi ya kawaida,tumecheza ingawa kipindi cha kwanza walituzidi lakini kipindi cha pili tulicheza sawasawa na bahati ikawa yao wamepata ushindi”.

Timu ya Mafunzo sasa wamefikisha alama 29 wakiwa nafasi ya nne 4, na Chuoni wapo nafasi ya kumi 10 na alama 22.

Chanzo: Salma Sports Media

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.