riadha

MBIO ZA NGORONGORO KUHAMISHIWA MEI


MBIO za Ngorongoro zilizokuwa zikifanyika wiki ya pili ya Aprili ya kila mwaka, kuanzia mwakani zitafanyika Mei ili kukwepa mvua za masika, imeelezwa.

Mwaka huu mbio hizo zilifanyika Aprili 16 huku mvua kubwa ikinyesha, ambapo aliyekuwa mgeni rasmi Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe alishauri mbio hizo kufanyika Mei ili kukwepa adha ya mvua za masika.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mmoja wa waratibu wa mbio hizo, Meta Petro alisema waandaaji wamekubali ushauri wa waziri na kwamba mwakani mbio hizo zitafanyika Mei 13. Alisema angalau Mei mvua zinakuwa zimepungua na hivyo wameamua mwakani zifanyike Mei.

Alisema mwaka huu walipata shida baada ya mbio hizo za kilomita 21, tano na zile za watoto wa shule za msingi na sekondari kufanyika huku mvua kubwa ikinyesha.

Aidha, katika mbio za mwaka huu Ismail Juma aliibuka wa kwanza kwa upande wa wanaume wakati Fainuna Abdi alimaliza wa kwanza kwa upande wa wanawake. Washindi wa kwanza kila upande kila mmoja aliondoka na zawadi ya Sh milioni 1 wakati wa pili Sh 500,000.

Chanzo: Habari leo

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.