Timu ya polisi bado ipo katika wakati mgumu katika ligi kuu ya Zanzibar kanda ya Unguja baada ya jana kutoka sare ya bila ya kufungana walipocheza na majeshi wa Kipanga katika mchezo uliosukumwa ndani ya dimba la Amani majira ya saa kumi za jioni.
Licha ya timu hizo kucheza mchezo mzuri lakini walizipoteza nafasi nyingi ambazo wamezipata kwani wachezaji hao hawakuwa makini kabisa katika umaliziaji wao, na kupelekea kumalizika kwa mtanange huo bila ya bao lolote kwa pande zote.
Ali Suleiman Mtuli, kocha wa timu ya Polisi amesema kuwa, “Tatizo kama mlivoliona bado sijawa makini katika kuzitumia nafasi, tunapata nafasi nyingi, timu inatengeneza nafasi nyingi sana lakini bado tunapoteza nafasi, icho ndo kilio chetu Polisi kwa sasa”.
Aidha Mwenyekiti wa timu ya Kipanga Meja Shamhuna amesema, “Mechi ya leo vijana wamecheza vizuri wamejitahidi na tumetengeza nafasi nyingi tu lakini kwa bahati mbaya ma forward hawakuzitumia vizuri, na hiyo inatokana na part of the game unaweza unaweza ukapata nafasi nyingi na msizitumie au mkapata nafasi moja mkaitumia hiyo hiyo, ni hali ya mchezo”.
Kwa matokeo hayo Kipanga wamefikisha alama 24 wakiwa nafasi ya nane 8, na Polisi wapo nafasi ya pili kutoka chini ambayo ni nafasi ya kumi na tatu 13 na alama kumi 10.
Chanzo: salma sport's media
0 comments:
Post a Comment