ASFC

VURUGU ZAPELEKEA MCHEZO KUSHINDWA KUMALIZIKA, HATMA YA YANGA NDANI YA TFF


Kamati husika ndani ya shiorikisho la soka nchini TFF, ndio itakao amua mshindi wa mchezo wa nusu fainali ya kombe la TFF kati ya yan ga na coastal union baada ya leo kushindwa kumalizika.

Mchezo huo ulishindwa kumaliza dakika 120 baada ya mashabikia kuanza kurusha chupa na mawe uwanjani wakionekana kutoridhishwa na maamuzi ya mwamuzi wa mchezo huo.

Katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Mkwakwani ulishuhudia dakika 45 za kwanza zinamalizika kukiwa hakuna timu iliyoshuhdia nyavu za mpinzani wake.

Katika kipindi cha kwanza ynaga na coastal union walikuwa wnashambuliana kwa kasi, hiuku kila upande ikipoteza nfasi za kujipatia magoli.

Katika kipindi cha pili Coastal union walifanikiwa kuandika goli la kwanza kupitia kwa Yusuf Sabo katika dakika ya 54 kabla ya Donald Ngoma kuisawazishia yanga katika dakika ya 60.

Goli la Donald Ngoma lilionekana kupingwa na wachezaji wa coastal union pamoja na mashabiki wao wakiamini mfungaji Donald Ngoma alikuwa ameotea.

Mashabiki wa Coastal walipeleka mchezo kusimama kwa muda wa dakika 5 kabla ya mwamuzi kuamuru mchezo kuendelea na kupeleka dakika 90 zikimalizika kwa sare ya 1-1.

Katika dakika ya za nyongeza Yanga SC waliandika goli la kuongoza katika dakika ya 97 kupitia kwa Amisi Tambwe, goli liliopingwa vilivyo na mashabiki wa Coastal union na baada ya kumalizika dakika 15 za mwanzo, mchezo ulishindwa kuendelea kutokana na fujo kuendelea.

Fujo hizo zilipeleka kushindwa kuendlea kwa mchezo huo na kuvunjika mara baada ya dakika 15 za mwanzo kumalizika.

Kutokana nahali hiyo kunapeleka maamuzi ya timu ipi kati ya yanga na coastal union itakayo pita na kutinga fainali ya michunao hiyo itaamuliwa na kamati husika ya TFF.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.