VPL

HATIMA YA TANGA SASA MKONONI MWA AZAM FC, MGAMBO WAICHAPA JKT RUVU


Unaweza kusema hatima ya timu mbili za Tanga kusalia ligi kuu ya vodacom zipo mkononi mwa Azam FC baada ya leo Mgambo JKT kubuka na ushindi wa goli 1-0 mbele ya JKT Ruvu.

Mgambo JKT leo walikuwa wenyeji wa JKT Ruvu katika uwanja wa CCM Mkwakwani mchezo ambao ulikuwa muhimu kwa pande zote mbili kukwepa kushuka daraja.

Goli Lambart Sabo Lukindo katika kipindi cha pili imepelekea Mgambo JKT kuvuna pointi tatu hii leo na kusubiri hatima yao katika mchezo dhidi ya Azam FC, mchezo wa kukamilisha msimu wa ligi kuu ya vodacom utakao fanyika Azam complex.

Wakati Mgambo wakiwka katika nafasi ya 13 baada ya ushindi wa leo, jirani zao African  Sport wao wameshuka mpaka nafasi ya 14 na kesho watakuwa na kibarua cha kutfuta pointi tatu kwa Azam FC na kama watafungwa mchezo huo, African sports itakuwa ashiria kuifuata nyayo za coastal union ambao teyari wamesha shuka.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.