ZGPL

MAFUNZO YATOA MAFUNZO KWA JANG'OMBE, KIJICHI IKILALA KWA KIPANGA


Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Zanzibar timu ya Mafunzo imewapa kichapo timu ya Jang’ombe boy’s cha mabao 3-1,katika mchezo wa ligi kuu uliosukumwa ndani ya uwanja wa Amani mjini Unguja.

Katika mchezo huo uliosukumwa majira ya saa kumi za jioni, Mafunzo walianza kushinda bao la kwanza lililofungwa na Hassan Ahmad dakika ya 29, dakika chache tu baadae Sadik Habib akaipatia Mafunzo bao la pili alilofunga katika dakika ya 34.

Ilipofika dakika ya 41 mchezaji wa Jang’ombe boy’s, Hafidh Bariki akaachia shuti kali lililomshinda mlinga mlango wa Mafunzo Abdul-swamad Suleiman,  mpira huo uliingia wavuni na kuipatia jang’ombe bao la kwanza.

Mafunzo walijipatia bao la tatu katika dakika ya 65 lililofungwa na Shaban Ali, na mchezo huo kumalizika kwa Mafunzo kuibuka na ushindi mnene wa mabao 3-1.

 Mafunzo sasa wamepanda hadi nafasi  ya pili wakiwa na alama 38, na Jang’ombe boys wapo nafasi ya kumi 10 na wana alama 25.

Katika mchezo mwingine Timu ya kijichi bado imeendelea kufanya vibaya katika mechi zake za ligi kuu ya Zanzibar kanda ya Unguja baada ya kupokea kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Wanajeshi wa Kipanga.

Mtanange huo uliosukumwa majira ya saa nane za mchana ndani ya dimba la Amani mjini Unguja,Kipanga walianza kufunga bao la mapema lililofungwa na Nassor Saleh katika dakika ya sita 6, Nassor akarudi tena wavuni kwa kufunga bao la pili mnamo dakika ya 31.

Ndani ya kipindi cha pili katika dakika ya 67 Imran Abdul Rai akaipatia Kipanga bao la tatu 3, na mpira ilimalizika kwa Kijichi kubamizwa kichapo cha mabao 3-0, kutoka kwa Wanajeshi hao wa Kipanga.

Kijichi ni mechi yao ya 21, wakiwa wameshinda michezo miwili, sare michezo tisa 9, na wamepoteza michezo kumi 10, wanashika nafasi ya 12, na alama 15.

Kwa upande wa Kipanga wao pia ni mchezo wa 21, wameshinda mechi saba 7, wamepoteza michezo mitano, na sare michezo tisa 9, wanakamata nafasi ya saba 7, na wana alama 30

Chanzo: SALMA SPORTS MEDIA

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.