Kwa ushindi huo ambao Genk wameupata hii leo umepelekea kufuzu kwa matokeo ya jumla ya goli 5-3 baada ya kukubali kichapo cha goli 2-0 katika mchezo wa awli uliochezwa siku ya ijumaa.
Mchezo huo wa leo ulikuwa mchezo wa mchujo wa kusaka nafasi ya mwisho kuiwakilishi Ubelgiji katika michuano ya Europa league ambayo bingwa wake ni Sevilaa ya Hispania.
Samata allifungia Genk goli la pili katika mchezo huo wa leo katika dakika ya 27 baada ya Mgiriki, Nikolaos Karelis kuipatia Genk goli la kuongoza katika dakika ya 20 kwa mkwaju wa penati.
Goli la tatu la Genk hii leo lilifungwa na Sandy Walah katika dakika ya 45 huku goli pekee la Sporting Charleroi likigfungwa na Jeremy Perbet katika dakika ya 40 na kupelekea mchezo kwenda mapumizko Genk wakiwa mbele kwa goli 3-1.
Nikolaos Karelis aliifungia tena Genk goli la 4 na 5 katika dakika ya 56 na 71 na kupelekea mchezo kumalizika kwa Genk kuibuka na ushindi wa goli 5-1..
0 comments:
Post a Comment