CECAFA

SIMBA SC KUREJEA KAGAME, AZAM FC IKTETEA UBINGWA WAO DAR


Simba SC wanatarajiwa kurejea katika michuano ya klabu bingwa Afrika mashariki na kati (Kombe la Kagame) ambapo Azam FC watakuwa na kibarua cha kutetea taji hilo hapo julai 16 jijini Dar es salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyowekwa katika mtandao wa Azam FC (www.azamfc.co.tz) michuano ya mwaka huu ya Kagame yanatarajiwa kufanyika nchini julai 16-30, ambapo Azam FC anaingia kama bingwa mtetezi.

Kwa mujibu wa kanuni za kombe hilo zilizo kuwa zinatumika katika miaka ya nyuma, kama nchi mwenyeji wa mashindano hayo ndiyo anapotoka bingwa mtetezi, basi nchi hiyo itakuwa na wawakilishi watatu katika michuano hiyo.

Kwa muntahadha huo Tanzania bara inatarajiwa kuwakilishwa na timu tatu ambapo Yanga anaingia kama bingwa wa Tanzania bara na Azam FC anaingia kama bingwa wa michuano hiyo, na hivyo kutoa fursa kwa simba ambaye ameshika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi msimu wa 2014/15.

Hapo awali ilitangazwa michuano hiyo ingefanyika visiwani Zanzibar na kwa mujibu wa taarifa hiyo ambao azamfc.co.tz umetoa kuwa wamearifiwa na TFF, kuwa michuano hiyo itafanyika jijini Dar es salaa.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.