mtazamo

SOKA LETU HALITAMBUI UWEPO WA SHABIKI

Nina mshangaa yule anaeshangaa maamuzi ya Ndanda FC kuikubali ombi la yanga kucheza mchezo wake wa nyumbani dhidi yanga katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

Ninashangaa zaidi kusikia vilabu vinalalamika kutoungwa na mashabiki kwa kujitokeza viwanja pale wanapocheza katika michezo yao mbali mbali.

Na ninaamini utanishangaa zaidi nikisema soka letu la bongo alitambui uwepo wa mashabiki, na halijui dhamani wanayo poteza kutotambua uwepo wa mashambiki.

Ligi yetu kwa sasa huenda ikawa ni ligi yenye mashabiki wengi kulinganisha na ligi za majirani zetu, lakini bado vilabu, bodi ya ligi na shirikisho la soka nchini hawatambui uwepo wao.

Uwingi wa uhitaji wa kuifuatilia ligi yetu ndicho kilichompelekea mfanyabiashara maarufu nchini Said Salim Bakharesa kuamua kuitumia kuteka soko la kingamuzi nchini.

Wakati timu ya watu wanaomzunguka mfanyabiashara huyo kuona fursa hiyo, vilabu, bodi ya ligi na shirikisho la soka nchini bado wakiwa hawatambui uwepo wa hao mashabiki ambao mzee huyo ameiona.

Kutokana na kutotambua uwepo wa mashabiki na kushindwa kuelewa mashabiki wanataka nini, ndipo unakuta mechi zinazowagusa mashabiki wengi nchini zinachezwa siku moja saa moja, ikiwa ndio mwanzo wa msimu.

Ratiba ya msimu huu unaoelekea mwishhoni kilichozingatia zaidi ni upatikanaji wa uwanja unaotakiwa kutumika kwa mechi husika.

Katika nchi kama hii ambao mashabiki wengi wasoka wamegawanyika katika makabila mawili Simba na Yanga, alafu unakuta michezo inayo husisha timu hizo zinacheza wakati mmoja.

Mazingira ya viwanja vinavyotumika ukiachilia mbali eneo la kuchezea ambalo bodi ya ligi na shirikisho la soka nchini linalitolea macho na kusahau eneo la mashabiki.

Katika baadhi ya viwanja nchini kwenda kuangalia mechi zake ni mateso kwa mashabiki, wala sio kivutio kwa mashabiki.

Kuchezewa kwa ratiba ya ligi bila sababu za kueleweka, kuhama hama ovyo viwanja katika msimu mmoja wa ligi nimiongoni mwa mambo yanayopelekea niamini kuwa bodi ya ligi, vilabu bado havitambui uwepo wao.

Toka ni usikie uwanja wa Manugnu Complexs siamini kama wanashindwa kuzungusha majukwaa ya yenye kuweza kuruhusu kuingiza mashabiki 5000-10000, hata kukuliuza jina la uwanja, kwa kuwa Mtibwa sugar ni miongoni mwa timu zilizojijengea ngome katika ligi kuu, na kulazimisha SImba na yanga kufika Manungu complex, wakati huo ukiwa katika ubora wake.

Timu kama Simba na yanga ambayo mazoezi ya timu hizo mashabiki wanajitokeza kuyaangaliwa wameshindwa kujitenegenezea maeneo rasmi ya kufanyia mazoezi, ambpo yangezungukwa na mabango ya matangazo.

Hivyo hyvyo ndicho kilichoplekea Ndanda FC kuwa wepesi kukubali kuhceza Taifa katika mechi ambayo wao ni wenyeji, wakati mashabiki wake wanao udhuria katika michezo yao kwa asilimia kubwa wakishindwa kushuhdia timu yao katika uwanja wa Nangwanda msimu huu ikicheza na yanga.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.