Mabingwa wa ligi kuu ya vodacom Yanga SC wameendeleza ubabe kwa Azam FC katika michezo ya fainali baada ya leo kuifunga Azam FC goli 3-1, katika mchezo wa fainali wa kombe la shirikisho la soka Tanzania (Azam Sports Federation Cup) na yanga kuibuka bingwa wa kombe hilo.
Katika mchezo wa leo Yanga SC walikuwa wa mwanzo kupata goli kupitia kwa Amisi Tambwe katika dakika ya 9 akimalizia krosi ya Juma Abdul na kuipeleka yanga maopumziko wakiwa mbele kwa goli 1-0.
Katika dakika 5 za mwanzo Azam FC walionekana tishio zaidi lakini kadri ya muda ulivyo kuwa unasogea ndio Yanga wakazidi kuwa hatari zaidi na utawala wa mchezo ukiamia kwa yanga sc.
Katika kipindi cha pili Yanga Sc walireja na kasi waliyomalizia katika kipindi cha pili na kufanikiwa kuandika goli la pili katika dakika ya 47 kupitia kwa Amisi Tambwe.
Dakika moja mbele Dider Kavumbagu aliiandikia Azam FC goli pekee katika mchezo huo kabla ya Deusi Kaseke kuhitimisha katika dakika ya 80 na kupelekea mchezo kumalizika kwa yanga sc kuibuka na ushindi wa goli 3-1.
Tuzo ya mchezaji bora wa michuano imeenda kwa Juma Abduli huku kipa bora ikienda kwa Aishi Manula na mfungaji bora kuchuka Atupele Green.
0 comments:
Post a Comment