CECAFA

YANGA YATIBUA MIPANGO YA AZAM FC KUTETEA TAJI LAO MWAKA HUU, TFF YAJITOA

Azam FC walipo twaa taji la klabu bingwa Afrika Mashariki mwaka jana jijini Dar es salaam
Kuna dalili za Azam FC kushindwa kutetea taji lake la kombe la Kagame mwaka huu kutokana na kuwepo kwa uwezekano wa kombe hilo kutofanyika kwa mwaka huu, baada ya shirikisho la soka nchini TFF kuitolea nnje CECAFA.

Hapo awali michuano hiyo ilitakiwa kufanyika katika visiwa vya Zanzibar, kabla ya kujitoa na baraza lasoka Afrika mashariki na kati (CECAFA) kuiomba TFF iandae ambapo nayo imethibitisha kuto weza kuaanda kutokana na yanga kuwa na ratiba ya kuiwakilisha nchi katika michuano ya CAF.

BOIPLUS blog imemnukuu Ofisa habari wa shirikisho hilo Alfred Lucas akisema wamefikia hatua ya kukataaombi la CECAFA kutokana na ratiba ya mechi za kimataifa ya timu ya Taifa na klabu ya Yanga ambao wameingia katika hatua ya makundi ya kombe la shirikisho barani Afrika hivyo wakiwa waandaji watashindwa kuwahudumia ipasavyo wageni wataokuja.

" Ni rasmi kwamba hatutaandaa michuano ya kombe la Kagame kutokana na muingiliano wa ratiba ya michuano hiyo na mechi za kimataifa za klabu ya Yanga na timu ya Taifa hivyo itakuwa ngumu kwetu, tumewaandikia barua CECAFA kuwajulisha juu ya hilo," alisema Alfred.

Vilevile blog ya salehjembe imemnukuu raisi wa shirikisho la soka nchini TFF, Jamal Malinzi akisema: “TFF haikuwahi kusema itandaa michuano hiyo, ilikuwa chini ya Zanzibar ambayo imetangaza kujitoa. Maana yake mwanachama yoyote wa Cecafa anaweza kuingia na kusaidia."

“TFF iko katika wakati mgumu, moja ya timu, Yanga inashiriki michuano ya kimataifa na itacheza mechi mbili kwa mwezi, hakika itakuwa vigumu,” ilieleza sehemu ya kauli ya Rais wa TFF, Jamal Malinzi.

Endapo hakuto tokea kwa nchi mwanachama wa CECAFA atakae taka kuokoa jahazi ni wazi kwamba Azam FC watashindwa kutetea kombe lao hilo kwa mwaka huu.

Katika miaka ya hivi karibuni CECAFA wamekuwa wakiitumia Tanzania bara kuandaa michuano hiyo kila inapotokea aliyeomba kuanda michuano hiyo kujitoa dakika za mwisho kama ilivyo tokea kwa Zanzibar mwaka huu, hivyo kuna uwezekano mkubwa kutofanyika kama TFF wataendelea na msimamo huo wakuto andaa michuano hiyo.

Katika miaka ya hivi karibuni michuano ya kombe la Kagame limekuwa likipoteza mvuto na hivyo limekuwa alizivutii nchi wanachama kujitokeza kutaka kuandaa michuano hiyo mikubwa katika ukanda huu.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.