wanawake

23 WATAKAO WAVAA RWANDA WATAJWA

KOCHA wa Mkuu wa timu ya wanawake, ‘Twiga Stars’, Nasra Juma ametangaza kikosi cha wachezaji 23 watakaoingia kambini Julai mosi kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Rwanda.

Akizungumza na wandishi wa habari jana, Ofisa habari wa TFF, Alfred Lucas alisema kuwa timu hiyo itakuwa kambini kwa wiki mbili na itasafiri Julai 15 kwenda Rwanda na kucheza Julai 17.

“Kikosi hiki wiki ya kwanza kitakuwa kinafanya mazoezi na kurudi nyumbani na Julai 9-15 wataingia kambini kwenye hostel za shirikisho,” alisema Lucas.

Wachezaji walioitwa ni Fatuma Omar,Belina Julius, Najiat Abass, Anastazia Anthony, Stumai Abdalla, Fatuma Fatuma Idd, Fatuma Issa, Sophia Mwasikili, Donisia Daniel, Amina Ally, Shelder Boniface, Asha Rashid na Mwanahamisi Omar.

Wengine ni Happyness Henziron, Amina Ramadhan, Fatuma Bushiri, Wema Richard , Fadhila Hamadi, Mwajuma Abdallah, Anna Hebron, Johari Shabaan, Tumaini Michael na Maimuna Khamis.

Mchezo huo wa kirafiki utakuwa sehemu ya burudani kwa viongozi wa Afrika ambao wanahudhuria mkutano wa nchi huru za Afrika (AU) unaotarajiwa kuanzia Julai 14-18.

About Unknown

0 comments:

Powered by Blogger.