Wachezaji wa Faru Jeuri wakishangilia goli lao la kwanza |
Mabingwa watetzi wa kombe la Dr. Mwaka Sports Xtra Ndondo, Faru Jeuri wamefanikiwa kuwa wa mwanzo kutinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo baada ya leo kuibuka na ushindi wa goli 3-1 mbele ya Temeke Squad.
Faru Jeuri na Temek Squad wamekutana leo katika mchezo wa kwanza wa hatua ya mtoano wa michuano hiyo inayoendelea katika uwanja wa Bandari uliopo katika chuo cha Utalii.
Katika mchezo huo Faru Jeuri waliandika goli lao la kwanza katika dakika ya 7 kupitia kwa Masamaki Juma, baada ya kuoka shamulio la Temeke Squad.
Kipindi cha Kwnza Temeke Squad walitengeneza nafasi kadhaaa ambazo walishindwa kuzitumia huku wakitawala mchezona kupelekea mchezo kwenda mapumziko Faru Jeuri kuwa mbele kwa goli 1-0.
Katika kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Temeke Squad kusaka goli la kusawaizhsa huku Faru Jeuri wakisaka goli la kumaliza mchezo.
Katika dakika ya 61 Lambele Jerome aliiandikia goli la pili Faru Jeuri, goli lililopelekea Faru Jeuri kurudi nyuma kulinda goli lao huku wakipeleka mashambulizi ya kushtukiza kutafuta goli la 3.
Katika dakika ya 82 Faru Jeuri walipata penati baada ya mlinzi wa Temeke Squad kuushika mpira katika eneo la hatari, na Jerome Lambele kuifungia goli la 3 Faru Jeuri kwa mkwaju huo wa penati.
Katika dakika za nyongeza Temeke squad nao walipata penati na kuandika goli lao pekee katika mchezo huo kupitia kwa Twalibu Kabuluma, na kupeleka mchezo kumalizika kwa Faru Jeuri kuibuka na ushindi wa goli 3-1.
Katika mchezo wa leo Lambele Jerome aliibuka mchezaji bora, ambapo amezawadiwa elfu khamsini, tsheti na kofia ya Mwanaspoti, huku timu ya Faru Jeuri ikiondoka na laki tatu toka kwa Startimes na Temeke Squad ikiondoka na laki mbili toka kwa Startimes.
0 comments:
Post a Comment