Mchangani

TEMEKE MARKET WATINGA ROBO KWA MIKWAJU YA PENATI

Ibrahim Ajibu akishangilia goli la pili kwa timu ya Boom FC
Temeke Market wamefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya kombe la Dr. Mwaka linalosimamiwa na Sports Xtra na kudhaminiwa na gazeti la Mwanaspoti, Startimes, Azam TV na Dr. Mwaka, baada ya kuiondosha Boom FC kwa mikwaju wa penati 4-2.

Katika mchezo huo wa leo Boom FC walilazimika kumaliza dakika 55 wakiwa pungufu baada ya kipa wao kuzawadiwa kadi nyekundu katika dakika ya 40 ya mchezo.

Katika mchezo huo wa leo Temeke Market waliuwanza mchezo kwa kasi na katika dakika 4 za mwanzo walikuwa wanatawala mchezo kabla ya Ally Salum Kabunda kuwafungia Boom FC goli la kuongoza.

Kuingia kwa goli hilo kuliwachanganya Temeke Market na kupelekea Boom FC kurejea mchezoni na kupelekea mchezo kuwa sawa na mashambulizi yakeinda kila upande uku mpira mwingi ukichezwa katika eneo la kati la uwanja lililo kuwa linawakutanisha Abdallah Sesem na Abedi Kisiga upande wa Boom FC wakati upande wa Temeke Market ulikuwa unawakutanisha Shabani Kisiga na Abbas Kapombe.

Katika dakika ya 39 Temeke Market walipata penati iliyopigwa kwa ustadi mkubwa na Abbas Kapombe na mara baada ya penati hiyo kipa wa Temeke Market alizawadiwa kadi nyekundu kwa kosa la kurusha ngumi kwa mchezaji wa Boom FC na kupelekea mchezo kwenda mapumziko wakiwa sare ya goli 1-1.

Kipindi cha pili Boom FC walirejea kwa kasi na katika dakika ya 47 walifanikiwa kuandika goli la pili baada ya Abdallah Seseme kuitumia vyema pasi ya Ibrahim Ajibu na kuifungia Boom Fc goli la pili.

Kuingia kwa goli hilo kuliongeza kasi ya mchezo huku Boom FC wakicheza kwa nguvu na kutawala mchezo huku wakipoteza nafasi kadhaa za kufunga.

Katika dakika ya 75 Nassoro Kapama aliisawazihsia Temeke Market kwa kichwa akiunga krosi ya Julius Mrope na kupelekea mchezo kumalizika kwa sare ya goli 2-2.

Katika mikwaju ya penati Temeke Market walifanikiwa kufnga penati 4 wakati Boom Fc wakifunga penati 2 kati ya penati 4 walizopiga na kupelekea Temeke Market kuwa timu ya pili kutinga robo fainali.

Mchezaji bora wa mchezo wa leo ulienda kwa kiungo wa Boom FC Abedi Kissiga, aliyejizolea elfu hamsini, huku Boom Fc iklamba laki mbili na Temeke Mrket akichukuwa lati tatu.

About Unknown

0 comments:

Powered by Blogger.