wanawake

TWIGA STARS KUINGIA KAMBINI MWISHONI MWA WIKI

TIMU ya soka ya Taifa ya wanawake ‘Twiga Stars’ inatarajiwa kuingia kambini mwishoni mwa wiki hii kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya wanawake ya Rwanda.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Kocha Mkuu wa Twiga Stars, Nasra Juma alisema wamepata mwaliko Rwanda kwa ajili ya mchezo huo utakaochezwa Julai 17, mwaka huu.

Alisema leo atatangaza kikosi cha Twiga Stars ambapo kitaanza mazoezi ya siku tano kuanzia Ijumaa kisha baadaye kitaingia kambini kwa maandalizi ya mchezo huo.

“Tulipata mwaliko kwa wenzetu Rwanda, kwa hiyo tunajipanga kwa ajili ya kwenda kufanya vizuri, kikosi nitakitangaza kuanzia kesho (leo),” alisema.

Kocha huyo alisema Rwanda inataka kucheza na Twiga Stars kama sehemu ya kujipima kwa maandalizi ya michuano ya Afrika Mashariki.

Alisema wanachukulia mchezo huo ni muhimu kwao, ndio maana wanajipanga kufanya maandalizi ya kujiweka vizuri kwa ajili ya kupata ushindi.

Chanzo: Habari leo

About Unknown

0 comments:

Powered by Blogger.