Rais wa Shirikisho la Dunia la mchezo wa Karate (UPAM), Profesa Martina Maurizio (kulia), akiwaelekeza jambo wachezaji. |
BARAZA la Michezo nchini (BMT) limetangaza tarehe ya uchaguzi wachama cha mchezo wa JUDO ambao unatarajiwa kufanyika Agosti 8 mwaka huu huku nafasi mbalimbali za wagombea zikitangazwa na kuwataka klabu kujitokeza kuja kuchukua fomu zitakazoanza kutolewa kesho Juni 30 katika ofisi hizo.
Akizungumza na Michuzi blog , Afisa habari wa BMT Najaha Bakari amesema kuwa uchaguzi huo utafanyika hapa hapa Jijini Dar es salaam na kila klabu itatakiwa kutuma wawakilishi watatu wakiambatana na barua za utambulisho pamoja na cheti cha usajili wa klabu hiyo.
“kila Klabu inatakiwa kutuma wawakilishi watatu ambao wataingia kwenye mkutano mkuu wa mabadiliko ya katiba yatakayofanyika Agosti 5 ambayo ni siku moja kabla ya kufanyika kwa uchaguzi, ila wawakilishi hao wanatakiwa kuja na barua za utambulisho na cheti cha usajili wa klabu hiyo,”.
Ametaja nafasi zinazogombaniwa ni Rais, Makamu wa Rais, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu, Muhasibu, Mkurugenzi wa Ufundi ambapo gharama za uchukuaji wa fomu hizo itakuwa ni kiasi cha shilingi 20,000.
Katika nafasi yaKamishna wa waamuzi, kamati ya fedha na masoko, kamati ya kujitolea na ustawi na kamati ya elimu na michezo gharama yake itakuwa ni shilinngi 10,000 huku akiwataka wanachama waje kwa wingi kujchukua fomu kwani kila kitu kinahitaji waendeshaji ili kukijenga zaidi na kukiletea maendeleo pia amesema kuwa mwisho wa kuchukua fomu hizo ni Agostu 01.
"Fomu zote zitakuwa zinapatikana hapa na mwisho wa kuchukua ni Agosti 01 na kisha watafanya mchakato wa mabadiliko ua katiba na kisha kueleka siku ya uchaguzi ambapo utafanyika hapa hapa Jijini Dar es salaam ila sehemu husika haijajulikana bado,"amesema Najaha.
Chanzo: Michuzi Blog
0 comments:
Post a Comment