vilabu

MBEYACITY WAWEKA KAMBI MATEMA BEACH

Baada ya siku tano za mazoezi  kwenye uwanja wa Sokoine jijini hapa, kikosi cha mbeya city fc kimeondoka leo kuelekea wilayani Kyela kuweka kambi ya siku 10 ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya  kwa ajili ya msimu mpya  wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara  unaotaraji kuanza hivi karibuni.

Akizungumza na mbeyacityfc.com muda mfupi uliopita  Ofisa habari wa City, Dismas Ten, amesema kuwa  kikosi chao kimeondoka jijini Mbeya kikiwa na nyota 13 wa  zamani  pamoja na baadhi  wachezaji  wapya waliosajiliwa hivi pia  6 waliopandishwa kutoka timu ya Vijana.

“Ni kweli, tunaondoka leo kwenda wilayani Kyela kuweka kambi ya muda, kwenye kikosi tuko na nyota 13 wa zamani pia wachezaji wapya waliojiunga nasi  hivi karibuni na sijawasahau vijana wetu waliopandishwa kutoka timu ya vijana, wachezaji wetu wengine hasa waliokuwa nje ya jiji la Mbeya tunatarajia watajiunga nasi siku ya jumanne na kukamilisha idadi kamili ya kikosi chetu cha msimu ujao”

Akiendelea zaidi Ten alisema kuwa  kuhusu kujua nani na nani wapo kwenye kikosi na kina nani hawatakuwepo  ni vyema kusubiri kwa sababu siku chache zijazo taarifa hiyo itawekwa wazi na kocha kinnah Phiri ambaye anatarajiwa pia kuwasili siku hiyo ya jumanne.

“Mwalimu anatarajia kuwasili hapa jumanne akitokea Malawi kwenye mapumziko hivyo taarifa yake ya mwisho ndiyo itakuwa na majumuisho yote ya nani ni nani watakuwa sehemu ya kikosi msimu ujao”.

Kuhusu safari ya Malawi Ten alisema kuwa, bado City inasubiri  taarifa ya mwisho kutoka shirikisho la soka nchini humo ambalo liliomba kusogezwa mbele kwa ziara hiyo kupisha michezo ya timu ya taifa na pia vilabu vyao kwenye michezo mbalimbali ya kimataifa.

“Kama unavyofahamu ziara hii ilikuwa iwe mwezi juni lakini ilisogezwa mbele kupisha michezo ya timu ya taifa, bado tunasubiri taarifa yao ingawa sisi tuko tayari kwa zira hiyo kwa sababu taratibu zote tulishazikamilisha toka  ratiba ya awali”  alisema.

chanzo: mbeyacityfc.com

About dada

0 comments:

Powered by Blogger.