riadha

RIADHA WAKO TAYARI


WANARIADHA wanne wa Tanzania watakaoshiriki Michezo ya 31 ya Olimpiki itakayofanyika Rio, Brazil kuanzia Agosti 5 hadi 21 wako vizuri kiafya, imeelezwa.

Daktari wa timu hiyo ya Tanzania, Nassoro Matuzya alisema jana kuwa baada ya kuwafanyia vipimo wachezaji hao mjini Arusha, aliwakuta na matatizo madogo madogo, ambayo hayawezi kuwazuia kushiriki michezo hiyo.

Wanariadha watakaoshiriki Olimpiki baada ya kufuzu katika mbio za marathoni ni pamoja na Fabian Joseph, Alphonce Felix, Said Makuka na mwanadada pekee, Sarah Ramadhani.

Alisema kuwa matatizo aliyowakuta nayo ni yale ya maumivu madogo ya miguu kutokana na kutokimbia vizuri katika milima wakati wa mazoezi katika kambi yao ya West Kilimanjaro mkoa Kilimanjaro.

Matuzya akizungumzia hali ya Joseph ambaye hivi karibuni alikwenda jijini Dar es Salaam kwa matibabu ya mguu, alisema mchezaji huyo anaendelea vizuri na kwa sasa anafanya mazoezi pekee yake ili kuzidi kuimarika.

Alisema mwanariadha huyo alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya misuli ya mguuni na anaendelea vizuri kwa kufanya mazoezi peke yake kabla ya kuungana na wenzao. Alisema kuwa anasubiri awamu ya pili ya kuwapima wachezaji hao kabla ya kuwaruhusu kwenda kushindana Rio katika michezo hiyo ya Olimpiki.

Akizungumzia hali ya hewa ya West Kilimanjaro alisema kuwa ina tofauti kwani ni ya baridi wakati Rio kuna joto kali na alitoa ushauri wa kitaalamu, lakini kocha ndio huwa na uamuzi wa mwisho wa wapi kwa kupiga kambi.

Naye Kocha Mkuu wa timu hiyo, Francis John akizungumza kwa njia ya simu jana alisema hali ya hewa haitawaathiri wachezaji wake, ambao wataondoka nchi Agosti 16 wakati wengine watatangulia Agosti 2.

Chanzo: Habari Leo

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.