simba

SIMBA SC WATOA DOZI NZITO MORO, Mr. HAT-TRICK AKITUPIA MBILI


Mabingwa wa zamani wa ligi kuu ya Tanzania Bara Simba SC watoa kichapo kitakatifu kwa Polisi Morogoro katika mchezo wa kirafiki uliochezwa mkoani Morogro.

Katika mchezo huo kikosi cha kocha Joseph Omeg waliandika goli lao la kwanza katika dakika ya 5 kupitia kwa Fredrik Blagtnon kabla ya kurudi tena na kuiandika Simba SC goli la pili katika dakika ya 16 na kuipeleka Simba SC mapumziko wakiwa mbele kwa goli 2-0.

Katika kipindi cha pili Simba SC walirejea na kufanikiwa kufnga magoli manne na kupelekea mchezo kumalizika kwa Simba SC kuibuka na ushindi wa goli 6-0.

Alikuwa Ibrahim Ajib (Mr. Hat-trick) aliyefungua kalamu ya magoli katika kipindi cha pili alipoifungia Simba SC goli la 3 katika dakika ya 48 kabla ya kuifungia goli la 4 katika dakika ya 73.

Magoli mengine ya Simba SC yalifungwa na Abdi Banda katika dakika ya 85 na Mohammed Mussa katika dakika ya 82.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.