NAIBU Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Ackson amewaongoza Watanzania kushiriki mashindano ya riadha ya Tulia Marathon ya kilomita tano jana mkoani hapa.
Mashindano hayo yalianzia viunga vya Bunge mjini hapa na kuishia katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Mbali na Dk Tulia, wengine waliokimbia mbio hizo ni Waziri wa Kilimo na Uchukuzi, Dk Charles Tizeba, Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi, Kazi, Ajira na Vijana, Antony Mavunde, na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamadi Masauni.
Wengine ni wakuu wa mikoa ya Dar es Salaam, Paul Makonda na wa Simiyu, Antony Mtaka ambaye pia ni Mwenyekiti wa Riadha Tanzania (RT), Katibu wa (TOC), Filbert Bayi na wabunge kadhaa wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akizungumza baada ya kumaliza mbio hizo, Dk Tulia aliwataka Watanzania kuwakumbuka watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu kwa kuhakikisha kila mmoja anatimiza wajibu wake.
Awali akizungumza rais wa RT, Antony Mtaka alisema lengo la mashindano hayo ni kutafuta namna ya kupambanua wanawake wapya ndio maana wakayapa mashindano hayo jina la Naibu Spika.
Chanzo: Habari Leo
0 comments:
Post a Comment