TFF

AZAM WAICHAPA YANGA KWA MIKWAJU YA PENATI, YATWAA NGAO YA JAMII

Mabingwa wa Afrika mashariki na kati Azam FC wamefanikiwa kutwa ngao ya jamii kwa mara ya kwanza baada ya kuwafunga yanga sc kwa mikwaju ya penati 4-1, baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya ya goli 2-2.

Katika mchezo huo ulishuhudia Azam FC wakifanya shambulizi lao la kwanza katika lango la yanga katika dakika ya 30 ikiwa ni baada ya yanga kuwa mbele kwa goli 2-0.

Katika dakika zote 30 za mwanzo Yanga SC walitawala vilivyo mchezo na kufanikwa kupata magoli mawili yaliyofungwa na Donald Ngoma katika dakika ya 20 kwa mkwaju wa penati na 22 akimalizia pasi ya Hassan Kessi.

Katika kipindi cha pili Azam FC walianza kwa mabadiliko ya kumtoa Ramadhani Singano na kumuingiza Mudathir Yahya kitendo kilichorejesha mchezo kuwa sawa kwa pande zote mbili huku wakishambuliana kwa zamu.

Alikuwa Shomari Kapombe alieandikia Azam Fc goli la kwanza katika dakika ya 75 kabla ya John Bocco kuifungia Azam FC goli la kusawaizsha kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 90 na kupeleka dakika 90 kumalzika kwa sare ya goli 2-2.

Katika mikwaju ya penati Azam FC walipata penati zote nne wakati yanga wakipata penati moja iliyopigwa na Deo Munish Dida huku Haruna Niyonzima na Hassan Kessi wakikosa penati.

Penati za Azam Fc zilifungwa na Himid Mao, John Bocco, Michael Bolue na Shomari Kapombe wakipata penati za Azam FC

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.