CAF

SERNEGETI BOYS WAIONDOSHA AFRICA KUSINI WAICHAPA GOLI 2

Mohammed Rashid Abdallah akishangilia goli la kwanza la Sererngeti boys hii leo
Timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 Serengeti Boys wamefanikiwa kuwatoa Afrika kusinin kwa jumla ya magoli 3-1 baada ya leo kuibuka na ushindi wa goli 2-0 mchezo uliochezwa katika uwanja wa Azam complex hii leo.

Katika mchezo huo wa kusaka tiketi ya kwenda Madagascar mwakani kushiriki mashindano ya Afrika chini ya miaka 17, Serengeti boys waliuwanza mchezo kwa kasi na kujikuta wakipoteza nafasi ya kuandika goli la kuongoza katika dakika za mwanzo wa mchezo.

Alikuwa Mohammed Rashid Abdallah aliyeindikia Serengeti boys goli la kwanza katika dakika ya 33 goli lilodumu kipindi chote cha kwanza.

Katika dakika ya 44 kiungo wa Serengeti Boys Ng'anzi alizawadiwa kadi nyekundu ikiwa ni baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano.

Kipindi cha pili muda mwingi Serengeti Boys walikuwa wakilinda goli lao na kupeleka mashambulizi ya kushtukiza ambapo katika dakika ya 82 Muksin Makame aliiandikia Serengeti boys goli la pili na kupelekea mchezo kumalizika kwa Serengeti boys kuibuka na ushindi wa goli 2-0.

Matokeo ya leo ukiunganisha na matokeo ya mchezo wa awali uliochezwa Afrika kusini ambapo ulimalizika kwa sare ya goli 1-1, hivyo unaifanya Serengeti boys kuiondosha Afrika kusini kwa jumla ya magoli 3-1.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.