simba

SIMBA WAPOTEZA KWA KMC


Baada ya kupata ushindi katika michezo yake mitatu ya kirafiki, kikosi cha Simba SC kikiwa chini ya kocha Joseph Omeg leo imepoteza mchezo wake wa kwanza wa kirafiki kwa kufungwa goli 1-0 kutoka kwa KMC.

Goli pekee la KMC ya Kinondoni jijini Dar es salaam lilifungwa na Rashid Toshwa katika dakika ya 10 ya mchezo.

Simba SC wapo mkoani Morogoro kwa kambi maalumu ya maandalizi ya ligi kuu ya vodacom inayotaraji kuanza mwezi wa huu tarehehe 20.

Wakiwa Morogoro Simba SC imeshafikisha michezo minne ya kirafiki waliyocheza mkoani Morogoro, ambapo walianza kwa kushinda goli 6-0 mbele ya Polisi Morogoro, kisha kuifunga Burkinafaso ya Morogoro goli 5-0 kabla ya kushinda 2-0 mbele ya Moro kids na leo wakfungwa na KMC katika mchezo wao wa nne wa kirafiki.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.