Simba imeuanza msimu vizuri kwa utambulisho wa kikosi chake kwa kufunga mabao matatu katika mechi moja.
Simba imewatwanga wageni wake AFC Leopards ya Kenya kwa mabao 3-0 katika mechi ya kirafiki maalum katika Simba Day iliyopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mshambuliaji nyota wa Simba, Ibrahim Ajib aling’ara kwa kufunga mabao akianza na dakika ya 38 kwa kushuti kali nje ya 18 kabla ya kuandika la pili katika dakika ya 55.
Simba ilikwenda mapumziko ikiwa na mabao mawili lakini kipindi cha pili, mabadiliko yakaifanya kuwa bora zaidi na kufunga mabao mengine mawili kupitia kwa Shiza Kichuya na Laudit Mavugo akafunga la nne katika dakiaka ya 81.
Ivan Otieno, kipa wa AFC Leopards ndiye alikuwa kipingamizi kikubwa kwa Simba kufunga angalau mabao sita au saba.
Simba inayofundishwa na Joseph Omog raia wa Cameroon, ndiyo ilishambulia kwa kasi zaidi na kuwapa wakati mgumu Leopards waliokuwa wanaongozwa na Raphael Kiongera.
Chanzo : Salehjembe blog
0 comments:
Post a Comment