Beki wa kati wa George Osei ametemwa na klabu ya Ruvu Shooting ambayo tayari imeshatangaza nyota wake iliowasajili na kuwatema taya kwa ajili ya msimu wa VPL 2016/2017.
Osei anakumbukwa na wengi baada ya tukio la kumkaba shingoni mshambuliaji wa Yanga mrundi Amis Tambwe wakati wa mchezo wa ligi kuu Tanzania bara kwenye uwanja wa taifa kabla ya timu hiyo kutoka mkoa wa Pwani haijashuka daraja.
Timu ya soka ya Ruvu Shooting, imekamilisha usajili wa wachezaji wake watakaoichezea msimu mpya wa 2016/17.
Wachezaji wapya waliosajiliwa msimu huu, timu walizotoka kwenye mabano ni Jabir Aziz (Mwadui FC), Richard Peter (Mbeya City), Elias Emanuel (Polisi Morogoro), Clidel Loita (Mji Njombe), Chande Magoja na Fuluzuru Maganga wote kutoka Mgambo JKT, Shaibu Nayopa (Oljoro), Abrahaman Musa (JKT Ruvu) na Renatus Kisasa ambaye ni mchezaji huru.
Aidha wachezaji wazamani walioachwa ni Ally Khan, Yahya Tumbo, Chagu Chagula, Juma Mpakala, Rashid Gumbo, Kulwa Mobi, Gidion Seppo na George Osei.
Timu iko kambini Mabatini ikiendelea na mazoezi ambapo Agost 1, ilicheza mchezo wa kwanza wa kirafiki dhidi ya Mbeya City na kupata ushindi wa bao 1-0, leo Jumatano Agost 3 itakuwa uwanja wa Polisi College, Dar es salaam kucheza na Polisi Dar es salaam ambapo Jumamosi ijayo itakuwa Mabatini ikipambana na Azam FC.
Imetolewa na;
Masau Bwire
Afisa Habari na mawasiliano Ruvu Shooting.

0 comments:
Post a Comment