vilabu

KAULI YA MWADUI JUU YA UWAMUZI WA JULIO


Uongozi wa Mwadui FC umesema wao kama klabu bado hawajakaa kujadili uamuzi wa kocha wao Jamhuri Kihwelu Julio aliyetangaza kujiuzulu kufundisha soka nchini akitaja sababu ya kuchukua uamuzi huo ni waamuzi kutotenda haki.

Katibu Mkuu wa Mwadui FC Ramadhani Kilao amesema Julio anamaamuzi yake binafsi na wao kama uongozi watakaa na Julio na kufikia makubaliano.

“Julio anamaamuzi yake binafsi ambayo anayasimamia, sio jukumu letukumshawishi ila kuamua kwake kuachana na soka huo ni mtazamo wake. Sisi kama klabu kwetu haijawa rasmi, amerejea jana usiku tunategemea tutakuwa na kikao nae baada ya kikao hicho, tutakuwa na mtazamo wetu kama klabu,” amesema Kilao wakati akitoa kauli rasmi ya klabu kuhusu uamuzi wa Julio.

Kumekuwa na minong’ono kwamba Julio alipewa idadi ya mechi kuhakikisha anashinda la sivyo kibarua chake kingeota nyasi lakini hapa Katibu anafafanua: “Nimesikia wengi wanasema kwamba tulimpa mechi tatu ashinde, labda huko zinakotoka hizo taarifa wanajua lakini sisi kama klabu hatujawa na huo utaratibu.”

Chanzo : shaffihdauda.co.tz

About dada

0 comments:

Powered by Blogger.