VPL

YANGA WAICHALAZA JKT, WAKIKAA KILELENI


Magoli mawili ya Saimon Msuva na goli moja la kujifunga la Michael Aiden imepelekea Yanga SC kukaa kileleni mwa ligi kuu ya vodacom.

Mabingwa watetezi Yanga hii leo walikuwa wageni wa JKT Ruvu katika uwanja wa Uhuru mchezo uliomaizika kwa Yanga SC kuibuka na ushindsi wa goli 3-0.

Katika mchezo huo wa leo ndani ya dakika 30 za mwanzo ulionekana kuwa sawa kwa pande zote mbili huku wakishambuliana kwa zamu.

Katika dakika 38 pasi ndefu iliyomkuta Saimon Msuva na kujaribu kupiga krosi ambayo beki Michael Aidan alijikuta akijifunga akijaribu kuzia mpira usimfikie Deusi  Kaseke.

Kuingia kwa goli hilo kulipelekea JKT Ruvu kushindwa kutulia  na kupelekea safu yake ya ulinzi  kufanya  makosa  kadhaa ambayo Yanga Sc walish9indwa kuzitumia na kupeleka mchezo kwenda mapumziko Yanga wakiwa mbele kwa  goli 1-0.

Katika kipindi cha pili Yanga SC walitawala vilivyo mchezo na kutengeneza nafasi lukuki za kufnga mabapo walifanikiwa kuzitumia nafasi mbili.

Saimon Msuva aliiandikia Yanga goli la pili katika dakika ya 58 akimalizia krosi ya Deusi Kaseke baada ya Kaseke kupokea mpira safi kutoka nahodha wa leo kwa upande wa Yanga Haruna Niyonzima.

Pasi safi ya Haruna Ninyonzima inatumiwa vyema na Saimon  Msuva na kuiadikia yanga goli la  tatu katika dakika ya 90 na kupelekea  mchezo kumalizika kwa Yanga kuibuka  na ushindi wa goli 3-0.

Matokeo hayo yanifanya yanga kuongoza ligi kwa tofauti ya  pointi moja, wakiwa na pointi 36, huku Simba Sc wakiwa na pointi 35.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.