Ajali za mashabiki katika viwanja vya soka vimekuwa vikitokea Mara kwa Mara pale uwanja unapozidiwa na ukubwa wa mechi, na Mara nyingi husababishwa na uzidishwaji wa idadi ya mashabiki wanaotakiwa kuingia katika uwanja husika.
Shirikisho la soka nchini TFF Jana imetangaza Azam FC kutumia uwanja wake wa Azam complex katika michezo dhidi ya Simba na Yanga pale azam FC wanapokuwa wenyeji, ambapo uwanja unauwezo wa kubeba mashabiki wasio zidi 7000.
Kwa kuangalia uwitaji wa watu kushuhudia mchezo huo ni dhahiri idadi hiyo ni ndogo mno, ila Azam FC inaitaji kunufaika na uwanja wake wa nyumbani katika michezo ambayo anakuwa mwenyeji, hapo ndipo suala la uweledi ndipo linaitajika.
Kumekuwa na utamaduni wakuuza tiketi kuzidi uwezo wa uwanja ndio mara nyingi hupelekea uwanja kubeba idadi kubwa ya watu kulingana na uwezo wake. Hapo ndipo bodi ya ligi inatakiwa kuwa makini napo kuepusha majanga katika siku husika ya mchezo.
Ukiachana na kuuza idadi sahihi ya tiketi, vile vile bodi ya ligi inatakiwa kuhakikisha tiketi za mchezo wa Azam FC na Simba ama Yanga haziuzi uwanjani siku ya mchezo na ikiwezekana wafunge hesabu za uzwaji wa tiketi siku kabla ya mchezo husika.
Natumai wasimamizi wa ligi wakifanikiwa kusimamia hayo mechi zote zitakazochezwa Azam Complex zitamalizika salama bila ghasia ya aina yoyote ile, ile huku azam FC wakiendelea kunufaika na matumizi ya uwanja wao wa nyumbani na kuendelea kuwapa haki wadhamini wake wa uwanja, japo kuwa huwa wanatangaza bidhaa za wamiliki wa timu.
Ni wakati wa TFF kuonyesha uweledi wao katika masuala ya Tiketi na pongezi kwao kusikia kilio cha Azam FC cha mda wao na niwakati wa Mtibwa sugar na Mwadui kufikilia nini wanakosa kwa Simba na yanga kushindwa kufika katika viwanja vyao.
0 comments:
Post a Comment