Mchangani

WATANZANIA WASHIRIKI KWA MARA YA KWANZA MASHINDANO YA IUIU

Watanzania na Wasomalia wakisalimiana
Timu ya wanafunzi wa chuo cha kiislamu Uganda (IUIU) kampasi kuu (Mbale, Uganda) kutoka nchini Tanzania leo imecheza mchezo wake wa kwanza baada ya miaka si chini ya 15 kupita dhidi ya Somalia katika ligi inayo husisha mataifa yenye wanafunzi chuoni hapo nnje ya Uganda.

Katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa chuo hicho katika kampasi ya Mbale imeshuhudia Somalia wakitoka kifua mbele baada ya kuwafunga Tanzania goli 5-0, huku kiungo tegemeo wa Tanzania, ambaye ni mwenyekiti wa jumuiya ya wanafunzi wa Tanzania Said akiumia katika kipindi cha kwanza cha mchezo na nafasi yake ikachukuliwa na katibu wa jumuiya Alim Said "Bakayoko".


Somalia walienda mapumziko wakiwa mbele kwa goli 1-0, huku mchezo ukionekana kuwa uko sawa pande zote mbili, huku Tanzania wakifanikiwa kupata kona moja ambayo ilitokana na kupoteza nafasi kwa Tanzania kuandika goli kupitia kwa mshambuliaji wao Maulid.

Kipindi cha pili Tanzania walipoteana katika eneo la kati la uwanja na kuwafanya Somalia kutawala eneo hilo na kuwa chanzo cha Somalia kupata magoli mengine manne na kupelekea mchezo kumalizika kwa Somalia kushinda goli 5-0.

Tanzania wanataraji kucheza tena siku ya Jumapili dhidi ya Malawi, ambao wanaongoza kwa kuwa na pointi 3, sawa na Somalia na Nigeria wakipishana katika uwiano wa magoli ya kufunga na kufungwa. huku Kenya na Tanzania wakiwa hawajapata chochote huku wakiwa wameruhusu nyavu zao kuguswa mara 5 bila ya wao kugusa za wapinzani wao.
Kikosi cha Tanzania
Katika miaka hiyo 15 ambayo Tanzania walikuwa hawashiriki kutokana na idadi yao kuwa ndogo, walikuwa wakicheza chini ya kivuli cha Kenya (walikuwa wanaikiongezea nguvu kikosi cha Kenya). 

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.