CAF

YANGA WACHAPWA NA WABOTSWANA

Mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara Yanga SC wamejiweka katika mazingira magumu ya kuingia katika hatua ya makundi ya klabu bingwa Afrika baada ya leo kupitea kwa goli 2-1 mbele ya Township Rollers ya Botswana.

Yanga ili wapite katika hatua hii, ns kutings katika hatua ya makundi wanahitaji kushinda mchezo wa marejeano goli 2-0, mchezo utakaochezwa wiki ijayo jijini Gaborone, Botswana.

Katika mchezo wa leo uliochezwa katika uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam ulishuhudia wageni Township Rollers wakiwa wa mwanzo kupata goli kupitia kwa Lemponye Tshireletso katika dakika ya 11, akifunga kwa shuti la umbali wa mita 20.

Alikuwa Obrey Chirwa aliyeisawazishia yanga katika dakika ya 30 akimalzia pasi ya kiungo Papy Kabamba Tshishimbi, na kupelekea mchezo kwenda mapumziko wakiwa sare ya goli 1-1.

Kipindi cha pili Yanga SC waliingia kwa dhamira ya kusaka goli la pili, ambapo walijaribu kutengeneza nafasi kadhaa ambazo walishindwa kuzitumia, kabla ya Motsholetsi Sikele kuifungia Township goli la pili katika dakika ya 83 na kupelekea mchezo kumalizika kwa Yanga kufungwa goli 2-1.

Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Ramadhani Kabwili, Hassan Kessy, Gardiel Michael, Said Juma ‘Makapu’, Kelvin Yondani, Papy Kabamba Tshishimbi, Pius Buswita, Pato Ngonyani, Ibrahim Ajib/Juma Mahadhi dk68, Obrey Chirwa na Emmanuel Martin/Geoffrey Mwashiuya dk64.

Township Rollers; Keeagile Kgosipula, Maano Ditshupo, Mosha Gaolaolwe, Simisani Mathumo, Tshepo Motlhabankwe, Kaone Vanderwesthuisen, Motsholetsi Sikele, Lemponye Tshireletso, Segolame Boy, Mthokozisi Msomi/Ivan Ntege dk44 na Joel Mogorosi.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.