TAMASHA maalum linalo wahusisha wana michezo na wasanii waliowahi kusoma shule ya Sekondari Makongo ‘Makongo Day Bonanza’ linatarajiwa kufanyika jumamosi ya juni 18 katika viwanja vya Leader’s Club, Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, mratibu wa tamasha hilo Boniface PAwasa alisema lengo la tamasha ni kuwa kutanisha pamoja wanafunzi hao na wasasa, sambamba na kuhamasisha kuendeleza vipaji walivyonavyo.
Alisema, tamasha hilo pia lina lengo la kuwa hamasisha wanafunzo toka shule mbalimbali kujali na kuithamini michezo pamoja na sanaa nyingine kutokana na ukweli kwamba tasnia hiyo kwa sasa imeweza kutoa ajira kwa vijana.
Pawasa aliongeza kuwa kupitia tamasha hilo kuta kuwa na michezo mbalimbali ikiwemo soka itakayo husisha wachezaji nguli wa zamani walio soma shuleni hapo watakao kipiga na Yanga, huku kwa upande wa netiboli watapepetana na Bongo Movies.
Aliongeza kuwa pamoja na michezo hiyo kutakuwa na burudani toka kwa wasanii mbalimbali walio wahi kusoma Makongo pamoja na waliopo wakiwemo Dogo Janja, Mc Babu Ayoub, Seki, Bambo, Jose Mara, Kalala Junior na wengineo.
“Pia tumezialika shule mbalimbali kushiriki katika tamasha hilo zikiwemo Jangwani, Tambaza, Jitegemee, Tegete, Hazina International School, Kipingu Sports Academy na nyinginezo ambapo kiingilio kitakuwa sh.2000”, Alisema.
Baadhi ya wachezaji waliowahi kusoma makongo ni pamoja na Juma Kaseja, Mussa Mgosi, Nico Nyagawa, Jerry Tegete, Haruna Moshi, Yahaya Akilimali, Kandole Justine, Aron Nyanda, Ali Mayai, Muhaji Kampala, Mohamed Banka, Adam Matunga, Jemedary Said, Majuto Komu, Aman Simba, Ngawina Ngawina na wengineo.
Dina Ismail
0 comments:
Post a Comment