wanawake

Asha kuelekea Sweden

Mchezaji anaekipiga katika klabu ya Mburahati Queens pamoja na timu ya taifa ya wanawake Twiga Stars, Asha Rashid 'Mwalala' anatarajiwa kwenda nchini Sweden kwa ajili ya majaribio.
Asha anatarajiwa kuondoka nchini juni 5 mwaka huu, kwenda katika klabu ya soka ya AIK  nchini Sweden, ambao na mabingwa wa Sweden.
Mshambuliaji huyo amepata mwaliko huo baada ya wakala wake Damas Ndumbalo kutuma wasifu waka katika klabu 10 tofauti barani ulaya. Asha alijaribiwa katika klabu ya Atasehir Beredisor ya nchini Uturuki hivi karibuni.

Ndumbalo akizungumzia safari ya Mwalala alisema huu ni mwanzo na wako wengine watakao fuata na hana mashaka juu ya Mwalala na ana imani atafanikiwa na kuwa njia kwa wengine.
"Wapo wengi tunawatafutia timu nje huu ni mwanzo iwapo Mwalala atafanikiwa tutapeleka wachezaji wengi zaidi ambao baadae watakuja kuisaidia timu yetu ya taifa kwenye mashindano mbali mbali ya kimataifa kama ilivyo kwa kina Nizar Khalfan, Henry Joseph, Danny Mrwanda na Abdi Kassim ' Babi'. Mwalala ni mchezaji mzuri sina shaka naye, naamini atafanikiwa kufuzu majaribio yake na hiyo itakuwa njia ya kuwavuta na wengine kupata nafasi ya kwenda kucheza soka nje na kuinua soka la wanawake hapa nchi," alisema Ndumbalo.


aamsuni

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.