mtazamo

Azam tangaza dau la Ngassa

Miaka ya nyuma kulikuwa na winga machachari Tanzania Lunyamila alingara vilivyo na uzi wa yanga na ningumu kusahaulika kwa uimara wake, japo kuwa kipindi hiki cha karibuni ameibuka winga mwingine mwenye kasi na uwezo unaotaka kulingana na Lunyamila. Ni bwana mdogo Mrisho Ngassa, mchezaji aliyefananishwa na Theo Walcot na Kocha Arsene Wenger.
Ngassa tangu mzunguko wa pili wa ligi uanze amekuwa akitawala vyombo vya habari kwa uongozi wa yanga kutaka kumrudisha kundini. Taarifa hizo zimepamba moto katika vyombo vya habari, huku azam fc wakisema Ngassa auzwi.
Ngassa alijiunga Azam fc kwa kitita cha tsh mili 58 akitokea yanga mwaka jana na kusaini mkataba wa miaka mitatu ambao unasemekana analipwa mil 1.7 kwa mwezi. Ngassa anaonekana hana dhamira ya kuendelea kuitumikia klabu hiyo na hivyo kutaka kurejea Yanga.
Kutokana na kauli yake kwa waandishi wa habari na wachambuzi wa soka nchini, si oni aja ya Azam kuendelea kumngangania mchezaji ambaye ametamka dhahiri kuwa anataka kurejea Yanga. Azam inatakiwa kuwa wa ungwana, kama yanga walikubali kumuuza iweje nyie wenye nyota wanao fanana kiuchezaji na Ngassa.Cha kufanya Azam watangaze bei kama yanga wataiweza kuimudu wamchukue na wakishindwa abakie akiwa anafahamu kuwa klabu inayo muihitaji imeshindwa kufikia bei yake.
Nina imani Azam wanaweza kuendeleza ushindani na kuwa bora msimu ujao bila ya Ngassa japo kuwa msimu uliokwisha alikuwa lulu klabuni hapo.

aamsuni

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.