TFF

Copa coca cola kutimua vumbi juni 11

Mashindano ya soka chini ya miaka 17 copa coca cola ngazi ya Taifa inatarajiwa kuanza hapo juni 11 mwaka huu. Mashindano hayo yanausisha timu za vijana toka mikoa yote ya jamhuru ya muungano ya Tanzania.
Hapo awali kulikuwa na pendekezo la mashindano ya mwaka huu kufanyika katika vituo vya Arusha, Mwanza na Dar es salaam katika hatua ya makundi, lakini wamefikia maamuzi ya kufanyika katika kituo cha Dar es salaam pamoja na Kibaha, Pwani.

Timu shiriki zinatakiwa kuwasili katika shule ya sekondari ya Filbert Bayi iliyopo Kibaha mkoani Pwani, kuanzia Juni 6 mwaka huu, tayari kwa mashindano.
Katika mashindano ya mwaka huu kutakua na hatua tano, nazo ni hatua ya makundi, mtoano (16 bora), robo fainali, nusu fainali na fainali yenyewe.

Mashindano haya hutumika kuibuwa vipaji mbalimbali vya soka, na kubaadhi ya nyota wanangara katika ligi kuu ya Tanzania bara.


aamsuni
source: dina ismail

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.