Ilala wamefanikiwa kujizolea kifuta jasho tsh milion 10 baada ya kushika nafasi ya tatu. Ilala jana walicheza na timu ya mkoa wa Kagera katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu ambapo Ilala waliibuka na ushindi wa goli mbili kwa moja.
Katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, timu ya Ilala walikuwa wa mwanzo kujiandikia goli kwa mkwaju wa penati uliopigwa na Vedastus Foto katika dakika ya 25 ya mchezo.
Kagera walisawazisha goli hilo katika dakika ya 42 ya mchezo kupitia kwa Shamte Odiro baada kutokea patashika ya piga nikupe langoni mwa timu ya Ilala. Mpaka wanakwenda mapumziko kila timu ilikuwa ina goli moja.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu ya Ilala kulisakama goli la Kagera na mnamo dakika ya 47 timu ya Ilala ilijipatia goli la pili kupitia kwa Samwel Rogart baada ya kupiga shuti la mbali lililotinga moja kwa moja wavuni.
Hadi kipenga cha mwisho kinapulizwa Ilala 2 - Kagera 1, na Samwel Rogart aliibuka mchezaji bora wa mchezo huo, na kujinyakulia tsh laki moja.
aamsuni

0 comments:
Post a Comment