vilabu

Kikwete mgeni rasmi katika harambe ya Yanga

Rais Jakaya Mrisho Kikwete, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika harambee ya kuchangia ujenzi wa uwanja wa kaunda na jengo la mtaa wa Mafia.
Harambee hiyo itafanyika julai 7 jijini Dar es salaam ambapo klabu ya yanga imepanga kukusanya kiasi cha sh. bilioni 5. Bilioni 2 zitatumika katika jengo la Mafia na kingine kitakwenda uwanja wa Kaunda pamoja na hosteli.
Msemaji wa Yanga Louis Sendeu alisema jana jijini Dar es Salaam, wamemtumia Raisi Kikwete barua ya kuwa mgeni rasmi katika harambee hiyo. "Tumemwandikia barua mheshimiwa Rais wiki tatu zilizopita, hivyo tunatarajia atakubali ombi letu ili aweze kushiriki katika harambee hiyo," alisema Sendeu.
Alisema siku hiyo ya harambee wameandaa chakula cha jioni, ambapo kutakuwa na tukio la uchangiaji wa fedha kwa klabu hiyo kwa lengo la kufanikisha ujenzi wa uwanja na jengo lao. Sendeu alisema wameona ni vyema wakamshirikisha Rais kwa kuwa ni mtu anayependa maendeleo ya soka nchini na amekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha michezo.
Alisema pia watazialika kampuni, mashirika, wafanyabiashara maarufu nchini pamoja na wanachama ambao watakuwa tayari kuchangia, ili kufanikisha ujenzi huo. Kamati ya Ujenzi ya klabu hiyo, inaongozwa na Mwenyekiti wake, Mbaraka Igangula.


aamsuni
source: majira

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.