Mchangani

KILI TAIFA CUP 2011 kurindima leo Arusha

Michuano ya kili taifa cup 2011 itaendelea leo kutimua vumbi katika hatua ya robo fainal mkoani Arusha.
Michezo yote ya robo fainali mpaka fainali yenyewe itapigwa katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha, baada ya hatua ya awali kumalizika katika mikoa sita hapo mei 11.
Mchezo wa kwanza wa robo fainali utakutanisha kati ya Singida na Ilala utakao anza saa nane mchana wakati wa pili utakunisha mkoa wa Mwanza n Arusha.

Singida ambaye ni bingwa mtetezi atakuwa na kibarua kigumu mbele ya mkoa wa kisoka wa Ilala ambayo imeonyesha kuwa na ngome imara.
Ilala wanataka kurudisha heshima yao iliyopotea mwaka jana baada ya kushindwa kulitwa kwa mara ya tatu mfululizo baada ya kutolewa mapema.

Mshindi wa mechi za leo ataingia nusu fainali ambapo watakutana tarehe 24 mei katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.


aamsuni

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.