Klabu ya Azam fc inatarajiwa kuwapeleka walimu wawili watimu hiyo katika kozi ya awali ya ukocha itakayo fanyika hivi karibuni katika mji wa Birmingham.
Kuwapeleka walimu hao ni mikakati ya kuimarisha benchi la ufundi la Azam fc.
Makocha hao ambao watasomea kozi tofauti ni Kali Ongala atakayechukua mafunzo ya ukocha wa kawaida wakati Iddi Aboubakar Machumu atachukua mafunzo ya ukocha wa magolikipa.
Machumu ni miongoni mwanyota waliounda kikosi kilicho iwezesha Azam FC kupata nafasi ya kushiriki ligi kuu kwa mara ya kwanza wakati Kali alisajiliwa na Azam FC msimu uliopita akitokea Sweden na baadae kupewa nafasi ya ukocha msaidizi ambapo TFF walipinga kutokana na kutokuwa na sifa, na hivyo Azam FC kutangaza kuwa hakumpa ukocha usaidizi kama magazeti yalivyo ripoti, japo kuwa aliendelea kufanya kazi hiyo, huku akitambulika kama mchezaji.
Mkamu Mwenyekiti wa Azam FC, Said Mohamed amesema makocha hao wataondoka nchini siku chache kabla ya kuanza kwa mafunzo hayo yatakayofanyika katika chuo cha Birmingham Country For Development Scheme Ltd na yatachukua wiki mbili.
Azam FC inakuwa klabu ya kwanza kwa miaka ya hivi karibuni kupeleka na kugharamia makocha kusomea kozi hiyo.
Katika hatua nyingine Azam FC wanatarajiwa kuanza mazoezi ya kujiwinda na ligi kuu mwezi ujao tarehe 10, katika kituo chao cha Chamanzi.
aamsuni
source: azamfc.co.tz

0 comments:
Post a Comment