TFF

Makocha kuongezewa makali

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) kupitia Kurugenzi ya Ufundi limeandaa kozi ya ukocha ngazi ya daraja la juu itakayofanyika Dar es Salaam kuanzia Juni 6 hadi19.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana,  Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alisema kuwa jumla ya makocha 24 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara watashiriki  kozi hiyo.
Wambura aliwataja wakufunzi watakaoendesha kozi hiyo kuwa ni pamoja na Mkurugenzi wa Ufundi, Sunday Kayuni, kocha mkuu wa timu ya taifa, Taifa Stars, Jan Poulsen na Mjumbe wa Kamati ya Ufundi ya TFF, Salum Madadi.
Alisema kuwa kila mshiriki atalazimika kulipa ada ya sh50,000 kabla ya kuanza kozi na washiriki wanatakiwa kuthibitisha ushiriki wao kwa maandishi kabla ya Juni Mosi.
Wambura alisema washiriki watajitegemea kwa nauli ya kuja Dar es Salaam na kurudi pamoja na malazi wakati TFF itatoa chai na chakula cha mchana kwa kipindi chote cha kozi hiyo.  

Makocha walioteuliwa kushiriki ni Abdul Nyumba, Abubakar Balingula, Bakari Shime, Dady John, Emmanuel Makoye, Emmanuel Massawe, Fulgence Novatus, Ibrahim Mulumba, Juma Mgunda na Jumanne Mtambi. Wengine ni Leonard Jima, Leonard Barongo, Leticia Muganga, Lister Manyala, Maka Mwalwisi, Makoye Mayige, Nicholaus Achimpota, Oswald Mchopa, Peter Mhina, Salvatory Buchweishaja, Tiba Mlesa, Venance Kazungu, Victoria Chiefundo na Vitalis Salila.


mwananchi

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.