Mchangani

Mbeya yatinga fainali, kuwa vaa Mwanza

Timu ya mkoa wa Mbeya imefanikiwa kutinga nusu fainali baada ya kuichalaza mabao mawili kwa moja timu ya mkoa wa Kagera.
Katika mchezo huo wa nusu fainali ya pili uliupigwa katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Mbeya walikuwa wa Mwanzo kupata bao kwa mkwaju wa penati uliopigwa na Gaudence Mwaikimba mnamo dakika ya 24. Goli hilo lilidumu mpaka wanakwenda mapumziko.
Kipindi cha pili mnamo dakika ya 60 Kagera walisawazisha goli na kupelekea dakika 90 kuisha wakiwa sare ya 1-1.

Ndani ya dakika ya 3 katika dakika 30 za nyongeza, Mbeya walijiandikia goli la kuongoza baada ya mchezaji wa Kagera kujifunga katika harakati ya kuokoa. Mpaka kipenga cha mwisho wa dakika 30, Mbeya waliibuka kidedea kwa magoli mawili kwa moja.

Kutokana na matokeo hayo timu ya mkoa wa Kagera watacheza na Ilala hapo ijumaa ya mei 27 kutafuta milion 10, za mshindi wa tatu.
Wakati Mwanza na Mbeya watachuana jumamosi mei 28 katika mpambano wa kusaka mili 40 kwa bingwa wa michuano ya kili taifa cup 2010.


aamsuni

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.