wachezaji

Mgosi atingisha kiberiti

Mshambuliaji wa Simba aliyetuhumiwa kuhujumu timu na kupelekea kushindwa kutwa taji la ligi kuu, Mussa Hassan Mgosi aliliambia gazeti moja la Tanzania hapo juzi, kuwa hatoudhuria mazoezi mpaka aandikiwe barua ya kusitishwa kusimamishwa kwake.
Makamu mwenyekiti wa simba aliliambia gazeti hilo jana kuwa wamempigia simu Mgosi nakumuambia ajiunge na timu na akishindwa ajieleze kwa maandishi. Kitendo hicho kilipelekea Mgosi kuonekana Mazoezini jana lakini hakujiunga na timu na hivyo kufanya mazoezi kivyake vyake.
Mgosi ambaye mara kwa mara alijikuta akifungiwa na uongozi wa simba kwa utovu wa nidhamu, aliwasili katika mazoezi ya jioni uwanjani hapo akiwa amechelewa, alijifua peke yake pembeni na baada ya muda, alikwenda pembeni kupumzika huku akiwaacha wenzake wakiendelea.

Wachezaji wengine waliohudhuria mazoezi ya Simba jana ni pamoja na Juma Kaseja, Ally Mustafa ‘ Barthez’, Juma Jabu, Jerry Santo, Kelvin Yondani na Hilary Echesa. Wengine ni Nicco Nyagawa, Haruna Shamte, Amri Kiemba, Mohamed Banka, Juma Nyoso, Ali Ahmed Shiboli, Abdulhalim Humud, Aziz Gila, Shija Mkina, Uhuru Selemani, Amir Maftah, Samwel Temi pamoja na Athumani Iddi 'Chuji' aliyerejeshwa kundini akitokea yanga.
Simba wanajianda na mpambano wa klabu bingwa Africa dhidi ya Waydada ya Morocco utakaochezwa kati ya tarehe 27, 28 au 29 mei katika uwanja ulio huru utakao tangazwa hivi karibuni.


aamsuni

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.